National Development Plan
Permanent URI for this communityhttps://repository.mof.go.tz/handle/123456789/9
Browse
Browsing National Development Plan by Author "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania"
Now showing 1 - 20 of 21
- Results Per Page
- Sort Options
Item Hotuba Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23(Wizara ya Fedha na Mipango, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likae kama Kamati ya Mipango ili kupokea na kujadili mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23Item Maelekezo ya Makadirio ya Fedha za Matumizi ya Kawaida na ya Mpango Wa Maendeleo Kwa Mwaka 1999 - 2000(Ministry of Finance, 1999) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaItem Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019 -2020(Wizara ya Fedha na Mipango, 2019) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha wabunge wote kukutana tena hapa Jijini Dodoma, kupokea mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kwa mujibu wa Kanuni ya 97 fasili ya (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016. Aidha, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi yetu umoja na amani.Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023 -2024(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSerikali inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango Elekezi umegawanyika katika vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Kwa muktadha huo, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 ni ya tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.Item Mapendekezo ya Makadirio ya Matumizi ya Kawaida na ya Mpango Wa Maendeleo Kwa Mwaka Wa 2000 - 2001 (Kitabu Cha Pili)(Wizara ya Fedha, 2000) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaItem Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2013-2014(Wizara ya Fedha, 2014) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2015/16 ni ya Mpango wa mwisho katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Milano (2011/12 •2015/16) Iii kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa,2019(Wizara ya Fedha, 2019) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMapendekezo ya Mpango wa Maendele wa Taifa w.i Mwaka 2019/20 yanal enga kuweka msingi k wa ajili ya maandalizi ya Mpango wa Mwaka 2019/20. Lvlpango huo u takuwa wa nne katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Jvfae:ndeleo wa Miaka lvUtano,2 016/17- 2020/21, wenye clhima ya Kujenga Uchumi wa Viwanda iii Kuchochea Mageuzi ya Uch u,ni na Maendeleo ya 1-Vatu.Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2013 - 2014(Wizara ya Fedha na Mipango, 2013) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2013/14 ni ya pili katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Hivyo, mapendekezo hayo yanajikita katika kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano vifuatavyo: (i) Miundombinu ya nishati, usafirishaji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maji safi na maji taka na umwagiliaji; (ii) Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi ya viwandani, ufugaji, uvuvi na misitu; (iii) Viwanda vinavyotumia malighafi hususan za ndani na kuongeza thamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum za kiuchumi, kielektroniki na TEHAMA; (iv) Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.Item Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/2026(Wizara ya Fedha na Mipango, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambayo ni nyenzo ya kuunganisha juhudi za Taifa katika kufikia malengo ya maendeleo yanayotarajiwa ya kijamii na kiuchumi ilizinduliwa mwaka 1999. Uzinduzi huo ulifuatiwa na hatua za maboresho mbalimbali ya kisera, kitaasisi na kimfumo katika miaka ya 2000. Maboresho haya yalikuwa muhimu kutokana na hali ya kiuchumi ambayo Tanzania ilipitia katika miaka ya 1980 na 1990. Katika kipindi hicho, nchi ilikabiliwa na kiwango kidogo cha ukuaji wa uchumi, uhaba mkubwa wa bidhaa na huduma muhimu,mfumuko mkubwa wa bei, madeni makubwa na yasiyohimilika, na makusanyo madogo yamapato ya Serikali. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali ilichukua hatua kadhaa za maboresho ya kiuchumi kabla ya kuzindua Dira ya Maendeleo ya Taifa na mpango uliungwa mkono na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) uliojulikana kama programu ya maboresho ya mfumo wa uchumi (The Enhanced Structural Adjustment Facility - ESAF).Item Mapendekezo ya Serikali ya Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa 2021-2022(Wizara ya Fedha, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeloo wa Taifa wa Mwaka 2021./22 umeandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya MwalItem Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23(Wizara ya Fedha na Uchumi, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mpango huu umeandaliwa kwa lengo la kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ambayo ni kuiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ikiwa na sifa zifuatazo: maisha bora na mazuri; amani, utulivu na umoja; utawala na uongozi bora; jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi; na uchumi wenye uwezo wa kuhimili ushindani na kujiletea ukuaji wa kudumu kwa maslahi ya watu wote.Item Mkakati wa Serikali wa Kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kutekeleza Miradi yenye Kuchochea Upatikanaji wa Mapato ili ziweze Kujitegemea,2018(Wizara ya Fedha, 2018) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaNi lengo la serikali kuhakikisha kwamba mamlaka za serikali za mitaa zinaendelea kutumia fursa za kimapato zilizopo katika maeneo yaoItem Mpango wa Maendeleo wa Mwaka,1986 - 1987(Wizara ya Fedha, 1987) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaItem Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa 2014 - 2015(Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, 2014) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/15 ni wa tatu katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Hivyo, mpango huu unajikita katika kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano vifuatavyo: (i) Miundombinu ya nishati, usafirishaji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maji safi na maji taka na umwagiliaji; (ii) Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi ya viwandani, ufugaji, uvuvi na misitu; (iii) Viwanda vinavyotumia malighafi hususan za ndani na kuongeza thamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum za kiuchumi, kielektroniki na TEHAMA; (iv) Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017 - 2018(Wizara ya Fedha, 2017) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza umaskini.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2018 - 2019(Wizara ya Fedha, 2018) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa 2018/19 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2016/17 – 2020/21. Malengo mahsusi ya Mpango huu ni: (a) Kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kuongeza matumizi ya fursa na majaliwa ya kipekee ya nchi kwa tija; (b) Kuimarisha kasi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano, hasa kwa kutanzua changamoto za upatikanaji wa fedha na mitaji, ardhi na maeneo ya uwekezaji, na kuimarisha mipango miji na maendeleo ya makazi; (c) Kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani; (d) Kupanua fursa kuwezesha wananchi wengi kushiriki katika uwekezaji na uendeshaji biashara ili kuongeza uwezo wa nchi na wananchi kupambana na umaskini; (e) Kuimarisha ustawi na maendeleo ya jamii kwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji na kinga kwa jamii na kaya maskini; (f) Kuongeza idadi ya rasilimali watu yenye ujuzi na weledi unaohitajika katika uendeshaji wa uchumi wa viwanda na kuimarisha upatikanaji wa teknolojia na ubunifu na hivyo kujenga uwezo wa nchi kushindana kibiashara; na (g) Kuongeza uzalishaji katika sekta asili (primary production) ili kukidhi mahitaji na usalama wa chakula na upatikanaji wa mazao ghafi kwa uzalishaji viwandani kwa bei itakayowezesha ushindani kimataifaItem Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2012 - 2013(Wizara ya Fedha, 2012) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/13 unabainisha misingi, malengo, vipaumbele, mikakati ya utekelezaji, na changamoto zilizopo hivi sasa katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Aidha, Mpango umejikita katika kuwekeza kwenye maeneo ya kipaumbele ya kimkakati ambayo yataleta matokeo ya haraka katika ukuaji wa uchumi na kwa namna ambayo ni shirikishi.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017 - 2018(Wizara ya Fedha na Mipango, 2017) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya watanzania.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022 - 2023(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 ni wa Pili katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2021/22. Lengo la Mpango huu ni kuendeleza juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuweka mkazo katika ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya watu.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023- 2024(Wizara ya Fedha na Mipango, 2023) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Mwaka 2023/24 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango huu ni muhimu katika kuainisha maeneo mahsusi ya vipaumbele kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2023/24.