Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2024-2025
Abstract
Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali umeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mwongozo wa mwaka 2024/25 ni wa nne (4) katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Pamoja na mambo mengine, maandalizi ya Mwongozo huu yamezingatia: Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2020; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26); maelekezo mahsusi ya Serikali; na Agenda ya Afrika 2063. Lengo la Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali ni kutoa maelekezo kuhusu maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2024/25 kwa Maafisa Masuuli wote kuandaa mipango yao na bajeti kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa na kisekta pamoja na Sheria za Nchi, Kanuni, Nyaraka na Miongozo mbalimbali ya Kisekta na Serikali kwa ujumla.
Collections
- Budget Guidelines [36]