Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2025 - 2026
Abstract
Mwongozo wa Mpango na Bajeti umeandaliwa kwa mujibu wa Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mwongozo wa Mwaka 2025/26 ni wa mwisho katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 (TDV 2025) pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26. Maandalizi ya Mpango na Bajeti yamezingatia: Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi ya Mwaka 2020, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, Makubaliano ya Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Agenda 2063 ya Maendeleo ya Afrika, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 na maelekezo mahsusi ya Serikali. Lengo la Mwongozo wa Mpango na Bajeti ni kutoa maelekezo kwa Maafisa Masuuli wote kuhusu mambo ya kuzingatia wakati wa maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2025/26 .