Taarifa Fupi ya Kisera, 2022
Abstract
Sekta ndogo ya benki ni muhimu katika kutoa huduma mbalimbali ikiwemo kupokea na kutunza amana za wateja, kutoa mikopo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na kijamii na kuwezesha malipo mbalimbali. Sekta ya Benki nchini inaundwa na benki za biashara, benki za kijamii, benki za huduma ndogo za fedha, na benki za maendeleo. Sekta Ndogo ya Benki inaunda sehemu
kubwa ya sekta ya fedha a mbapo hadi kufikia Desemba 2020 ilikuwa inakadiri wa kuchangia asilimia 70 ya mali za sekta ya fedha. Kutokana na sekta ndogo ya benki kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini, Serikali imeku wa ikifanya maboresh o yakiwemomaboresho ya kwanza ( 1991- 2003) na ya pili ( 2006) ya sekta ya fedha ambayo yalilenga kuwezesha upatikanaji na utumiaji wa huduma za benki chini. Maboresho hayo yalisaidia kukua kwa sekta ndogo ya benki kulikochangi wanakuongeza kwa idadi ya taasisi za benki na kufikia 46 mwaka 2021 kutoka benki 10 miaka ya 1990.