Mwongozo wa Kitaifa wa Ufatiliaji na Tathmini ya Miradi na Programu za Maendeleo.
Abstract
Wizara ya Fedha na Mipango ina jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za ufauatiliaji na Tathmini(U&T) ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya miradi na programu za maendeleo kitaifa, Aidha, Wizara, Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa zina jukumu la kutekeleza shughuli za ufuatiliaji na Tathmini ya miradi na programu za kimaendeleo zinazotekelezwa na taasisi hizo katika maeneo husika. Hata hivyo, Uratibu wa shughuri za ufauatiliaji na tathamini wa miradi na programu za kimaendeleo umekuwa na changamoto mbalimbali zikiwemo: Miradi mingi kutokufanyiwa ufuatiliaji na tathmini, Kukosekana kwa taarifaza utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo, kukosekana kwa uwajibikaji katika ufuatiliaji na tathmini ya miradi na programu za maendeleo na Serikali kukosa taarifa na takwimu zenye ubora na kwa wakati kwa ajili ya kufanya maamuzi
Collections
- Budget Guidelines [33]