Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017 - 2018
Abstract
Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na
ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali
na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza umaskini.