Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023- 2024
Abstract
Mpango wa Mwaka 2023/24 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26, wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huu ni mwendelezo
wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango huu ni muhimu katika kuainisha maeneo mahsusi ya vipaumbele kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2023/24.