Hotuba ya Wizara ya Fedha na Mipango ya Makadirio ya Mapato na matumizi 2023 - 2024
Abstract
Mheshimiwa Spika, baada ya kupokea taarifa
iliyowasilishwa mbele ya Bunge lako Tukufu na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti,
Mhe. Daniel Baran Sillo – Mbunge wa Babati Vijijini,
naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako lipokee na
kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya
Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka 2022/23 na
kuidhinisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya
mafungu tisa (9) ya Wizara ya Fedha na Mipango,
pamoja na Fungu 45 - Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa
mwaka 2023/24.
Collections
- MoF Budget [21]