Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali Kwa Mwaka 2023 - 2024
Abstract
Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2023/24 umeandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti, Sura 439 na Kanuni zake za mwaka 2015. Uandaaji wa Mwongozo huu umefanyika kwa kurejea vipaumbele vilivyoainishwa kwenye dira, sera, mikakati na miongozo ya maendeleo kitaifa na kimataifa. Nyaraka zilizorejewa ni pamoja na: Mpango wa Maendeleo wa Taifa (2021/22 – 2025/26); Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020; Mpango Kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara; Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (2020/21 -2029/30); Sheria ya Bajeti, Sura 439; Sheria ya Madeni, Dhamana na Misaada, Sura 134; Sheria ya Fedha za Umma, Sura 348; Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410; Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa Awamu ya Tatu; Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030; Agenda ya Afrika Mashariki 2050; Dira ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika 2050; na Agenda ya Afrika 2063.
Collections
- Budget Guidelines [33]