Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
Abstract
Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22 unatoa maelekezo ya kuzingatiwa na Maafisa Masuuli wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma wakati wa uandaaji na utekelezaji wa mpango na bajeti. Mwongozo wa mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa kuzingatia matakwa ya Kifungu Na. 21 cha Sheria ya Bajeti, Sura 439.
Collections
- Budget Guidelines [33]