Ijue sheria ya Bajeti Namba 11 ya Mwaka 2015
Abstract
Sheria ya Bajeti Namba 11 ya Mwaka 2015 na Kanuni zake zilianza
kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2015. Tangu sheria imeanza kutumika
hadi sasa, kumekuwa na ongezeko la uhitaji wa wadau mbalimbali
kutaka kuifahamu sheria hiyo. Kutokana na mahitaji hayo, Serikali
imeona ni vyema kutoa chapisho hili la IjueSheria ya Bajeti Namba
11 ya Mwaka 2015. Lengo kuu la chapisho hili ni kujenga uelewa
juu ya sheria ya bajeti kwa umma na wadau wengine kwa ujumla.
Chapisho hili linatoa maelezo kwa lugha rahisi juu ya chimbuko la
sheria, sababu za kuwepo kwa sheria na mambo muhimu
yaliyozingatiwa kwenye sheria hiyo
Collections
- Budget Guidelines [33]