One-Year Development Plan
Permanent URI for this collectionhttp://10.1.67.219/handle/123456789/194
Browse
Browsing One-Year Development Plan by Subject "Pato la Taifa"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019 -2020(Wizara ya Fedha na Mipango, 2019) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha wabunge wote kukutana tena hapa Jijini Dodoma, kupokea mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2019/20, kwa mujibu wa Kanuni ya 97 fasili ya (1) na (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Januari 2016. Aidha, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuijalia nchi yetu umoja na amani.Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023 -2024(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSerikali inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango Elekezi umegawanyika katika vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Kwa muktadha huo, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 ni ya tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017 - 2018(Wizara ya Fedha, 2017) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza umaskini.