One-Year Development Plan
Permanent URI for this collectionhttp://10.1.67.219/handle/123456789/194
Browse
Browsing One-Year Development Plan by Subject "Miradi ya Maendeleo"
Now showing 1 - 3 of 3
- Results Per Page
- Sort Options
Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2017 - 2018(Wizara ya Fedha, 2017) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kupunguza umaskini.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2018 - 2019(Wizara ya Fedha, 2018) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa 2018/19 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2016/17 – 2020/21. Malengo mahsusi ya Mpango huu ni: (a) Kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kuongeza matumizi ya fursa na majaliwa ya kipekee ya nchi kwa tija; (b) Kuimarisha kasi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano, hasa kwa kutanzua changamoto za upatikanaji wa fedha na mitaji, ardhi na maeneo ya uwekezaji, na kuimarisha mipango miji na maendeleo ya makazi; (c) Kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani; (d) Kupanua fursa kuwezesha wananchi wengi kushiriki katika uwekezaji na uendeshaji biashara ili kuongeza uwezo wa nchi na wananchi kupambana na umaskini; (e) Kuimarisha ustawi na maendeleo ya jamii kwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji na kinga kwa jamii na kaya maskini; (f) Kuongeza idadi ya rasilimali watu yenye ujuzi na weledi unaohitajika katika uendeshaji wa uchumi wa viwanda na kuimarisha upatikanaji wa teknolojia na ubunifu na hivyo kujenga uwezo wa nchi kushindana kibiashara; na (g) Kuongeza uzalishaji katika sekta asili (primary production) ili kukidhi mahitaji na usalama wa chakula na upatikanaji wa mazao ghafi kwa uzalishaji viwandani kwa bei itakayowezesha ushindani kimataifaItem Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2012 - 2013(Wizara ya Fedha, 2012) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/13 unabainisha misingi, malengo, vipaumbele, mikakati ya utekelezaji, na changamoto zilizopo hivi sasa katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Aidha, Mpango umejikita katika kuwekeza kwenye maeneo ya kipaumbele ya kimkakati ambayo yataleta matokeo ya haraka katika ukuaji wa uchumi na kwa namna ambayo ni shirikishi.