National Development Plan
Permanent URI for this communityhttps://repository.mof.go.tz/handle/123456789/9
Browse
Browsing National Development Plan by Author "Jamhuri ya Muungani wa Tanzania"
Now showing 1 - 1 of 1
- Results Per Page
- Sort Options
Item Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050(2025-06) Jamhuri ya Muungani wa TanzaniaJamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja inayoundwa na Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, ikiwa na ukubwa wa eneo la kilomita za mraba (km ) 948,740, zikiwemo km 61,500 za maziwa na mito. Tanzania ipo katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, katika ukanda wa Maziwa Makuu ikipakana na Kenya na Uganda kwa upande wa kaskazini; Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa magharibi; Zambia, Malawi na Msumbiji kwa upande wa kusini; na Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki. Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, ilionesha kuwa Tanzania ina watu milioni 61.7, na hivyo kuwa miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu barani Afrika. Aidha, kwa mujibu wa sensa hiyo, asilimia 43 ya watu wote walikuwa na umri usiozidi miaka 15, kiwango kinachozidi wastani wa nchi za bara la Afrika ambao ni asilimia 41.