Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023 -2024
Abstract
Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango Elekezi umegawanyika katika vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Kwa muktadha huo, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 ni ya tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.