Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2012 - 2013
Abstract
Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2012/13 unabainisha misingi, malengo, vipaumbele, mikakati ya utekelezaji, na changamoto zilizopo hivi sasa katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Aidha, Mpango umejikita katika kuwekeza kwenye maeneo ya kipaumbele ya kimkakati ambayo yataleta matokeo ya haraka katika ukuaji wa uchumi na kwa namna ambayo
ni shirikishi.