Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022 - 2023
Abstract
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 ni wa Pili katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu ambao
utekelezaji wake ulianza mwaka 2021/22. Lengo la Mpango huu ni kuendeleza juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuweka mkazo katika ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya watu.