Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa 2014 - 2015
Abstract
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/15 ni wa tatu katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Hivyo,
mpango huu unajikita katika kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano vifuatavyo: (i) Miundombinu ya nishati, usafirishaji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maji safi na maji taka na umwagiliaji; (ii) Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi ya viwandani, ufugaji, uvuvi na misitu; (iii) Viwanda vinavyotumia malighafi hususan za ndani na kuongeza thamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum za kiuchumi, kielektroniki na TEHAMA; (iv) Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi, teknolojia na ubunifu na
kuimarisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.