Muongozo Wa Kujiunga Na Mfumo Wa GePG, 2017
Abstract
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, ikishirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), wametengeneza Mfumo wa Ukusanyaji wa Maduhuri uitwao kwa jina la “Government Electronic Payment Gateway (GePG)”. Mfumo huu umekamilika na tayari baadhi ya taasisi za serikali zimeunganishwa kwa majaribio. Aidha, watoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabenki na mitandao ya simu wameshirikishwa ili kufanikisha utekelezaji wa azma ya Serikali.
Collections
- GePG [11]