Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23
Abstract
Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mpango huu umeandaliwa kwa lengo la kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ambayo ni kuiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ikiwa na sifa zifuatazo: maisha bora na mazuri; amani, utulivu na umoja; utawala na uongozi bora; jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi; na uchumi wenye uwezo wa kuhimili ushindani na kujiletea ukuaji wa kudumu kwa maslahi ya watu wote.