Mkakati wa Ugharamiaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/262021/22 – 2025/26
Abstract
Utekelezaji madhubuti wa vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 - 2025/26 unahitaji rasilimali fedha kutoka vyanzo mbalimbali vya sekta ya umma na sekta binafsi. Mkakati wa Ugharamiaji umeandaliwa ili kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha za kutosha na kwa wakati kutoka katika vyanzo hivyo. Lengo kuu la Mkakati huu ni kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha zitakazowezesha kufikiwa kwa utekelezaji wa hatua za kimkakati na shabaha za Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano pamoja na kutanzua changamoto za ugharamiaji wa Mpango. Matokeo tarajiwa ni: kuimarika kwa upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka vyanzo vya ndani vya sekta ya umma na sekta binafsi; upatikanaji wa rasilimali fedha kutoka vyanzo vya kimataifa vya sekta ya umma na sekta binafsi; kuainishwa na kutumika kwa rasilimali fedha kutoka vyanzo bunifu; kuimarika kwa ushiriki na upatikanaji wa mitaji kutoka katika Asasi Zisizo za Serikali; na kuimarika kwa uratibu na uwianishaji wa mbinu na taratibu za ukusanyaji na upatikanaji wa rasilimali fedha.