Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II): Ni kwa Jinsi gani Tutaboresha Utekelezaji katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa?
Abstract
Mwanzoni mwa mwaka 2016, Serikali ilizindua FYDP II, kwa lengo la kurekebisha mapungufu ya FYDP I na kutoa mpango makini wakati Tanzania inapoanza kuelekea katika maendeleo ya viwanda katika miaka mitano ijayo (2016 – 2021). Katika kufanya marejeo ya FYDP I, serikali ilitambua kuwa mpango wa awali ulishindwa kufanikisha malengo yake mengi. Wakati Serikali imedhamiria kuwa ukuzaji wa viwanda ni kipaumbele katika miaka mitano ijayo, mapungufu ndani ya mpango unaweza kufanya nchi ishindwe kwa mara nyingine tena kama masuala yaliyojitokeza hayajafanyiwa kazi vya kutosha.