Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018
Abstract
Mwaka 2018, Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilifanya maboreshoya takwimu za Pato la Taifa kwa kutumia mwaka 2015 kama mwaka wa kizio kutoka mwaka wa kizio wa 2007. Kufuatia maboresho hayo, mabadiliko kadhaa yalijitokeza ikiwemo mfumo na ukubwa wa Pato la Taifa; viwango vya ukuaji na mchango wa sekta mbalimbali katika Pato la Taifa; na uwiano wa viashiria mbalimbali kwa Pato la Taifa. Maelezo ya kina kuhusu maboresho hayo yako katika sura ya kumi. Kutokana na zoezi hilo, kuanzia toleo hili takwimu zitakazotumika zitakuwa za mwaka wa kizio wa 2015. Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017. Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali
nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo. Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na: sanaa na burudani iliyokua kwa asilimia 13.7; ujenzi (asilimia 12.9); uchukuzi na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na habari na mawasiliano (asilimia 9.1).
Collections
- The Economic Survey [29]