One-Year Development Plan
Permanent URI for this collectionhttp://10.1.67.219/handle/123456789/194
Browse
Browsing One-Year Development Plan by Subject "Mpango"
Now showing 1 - 6 of 6
- Results Per Page
- Sort Options
Item Hotuba Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23(Wizara ya Fedha na Mipango, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likae kama Kamati ya Mipango ili kupokea na kujadili mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2013 - 2014(Wizara ya Fedha na Mipango, 2013) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2013/14 ni ya pili katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Hivyo, mapendekezo hayo yanajikita katika kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano vifuatavyo: (i) Miundombinu ya nishati, usafirishaji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maji safi na maji taka na umwagiliaji; (ii) Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi ya viwandani, ufugaji, uvuvi na misitu; (iii) Viwanda vinavyotumia malighafi hususan za ndani na kuongeza thamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum za kiuchumi, kielektroniki na TEHAMA; (iv) Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.Item Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23(Wizara ya Fedha na Uchumi, 2021) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na Sheria ya Bajeti, Sura 439. Mpango huu umeandaliwa kwa lengo la kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ambayo ni kuiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ikiwa na sifa zifuatazo: maisha bora na mazuri; amani, utulivu na umoja; utawala na uongozi bora; jamii iliyoelimika na inayopenda kujifunza zaidi; na uchumi wenye uwezo wa kuhimili ushindani na kujiletea ukuaji wa kudumu kwa maslahi ya watu wote.Item Mpango Wa Maendeleo Wa Taifa 2014 - 2015(Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, 2014) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2014/15 ni wa tatu katika mfululizo wa mipango ya kila mwaka ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16) ili kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. Hivyo, mpango huu unajikita katika kuendelea kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano vifuatavyo: (i) Miundombinu ya nishati, usafirishaji, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), maji safi na maji taka na umwagiliaji; (ii) Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara, malighafi ya viwandani, ufugaji, uvuvi na misitu; (iii) Viwanda vinavyotumia malighafi hususan za ndani na kuongeza thamani, viwanda vikubwa vya mbolea na saruji, viwanda vya kanda maalum za kiuchumi, kielektroniki na TEHAMA; (iv) Maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi kwa kutilia mkazo sayansi, teknolojia na ubunifu na kuimarisha mafanikio ya upatikanaji wa huduma za jamii; na (v) Uendelezaji wa huduma za utalii, biashara na fedha.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017 - 2018(Wizara ya Fedha na Mipango, 2017) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017/18 ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17 – 2020/21 na hivyo unaendelea kutekeleza maeneo manne ya kipaumbele ya: (i) Viwanda vya kukuza uchumi na ujenzi wa msingi wa uchumi wa viwanda; (ii) Kufungamanisha maendeleo ya uchumi na watu; (iii) Mazingira wezeshi kwa uendeshaji biashara na uwekezaji; na (iv) Usimamizi wa utekelezaji. Aidha, lengo kuu la Mpango huu ni kuhakikisha rasilimali na fursa za nchi zinatumika kujenga uchumi wa viwanda na kuboresha maisha ya watanzania.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022 - 2023(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 ni wa Pili katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2021/22. Lengo la Mpango huu ni kuendeleza juhudi za kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 kwa kuweka mkazo katika ukuaji wa uchumi, kupunguza umaskini na kuchochea maendeleo ya watu.