One-Year Development Plan
Permanent URI for this collectionhttp://10.1.67.219/handle/123456789/194
Browse
Browsing One-Year Development Plan by Subject "Maendeleo ya Taifa"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023 -2024(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaSerikali inaendelea na utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 wenye dhima ya Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu. Mpango huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inayotekelezwa kupitia Mpango Elekezi wa Muda Mrefu, 2011/12 – 2025/26. Mpango Elekezi umegawanyika katika vipindi vitatu vya miaka mitano mitano. Kwa muktadha huo, Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2023/24 ni ya tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26.Item Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2018 - 2019(Wizara ya Fedha, 2018) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMpango wa Maendeleo wa Taifa 2018/19 ni wa tatu katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2016/17 – 2020/21. Malengo mahsusi ya Mpango huu ni: (a) Kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa kuongeza matumizi ya fursa na majaliwa ya kipekee ya nchi kwa tija; (b) Kuimarisha kasi ya utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano, hasa kwa kutanzua changamoto za upatikanaji wa fedha na mitaji, ardhi na maeneo ya uwekezaji, na kuimarisha mipango miji na maendeleo ya makazi; (c) Kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani; (d) Kupanua fursa kuwezesha wananchi wengi kushiriki katika uwekezaji na uendeshaji biashara ili kuongeza uwezo wa nchi na wananchi kupambana na umaskini; (e) Kuimarisha ustawi na maendeleo ya jamii kwa kuongeza upatikanaji wa huduma bora za afya, elimu, maji na kinga kwa jamii na kaya maskini; (f) Kuongeza idadi ya rasilimali watu yenye ujuzi na weledi unaohitajika katika uendeshaji wa uchumi wa viwanda na kuimarisha upatikanaji wa teknolojia na ubunifu na hivyo kujenga uwezo wa nchi kushindana kibiashara; na (g) Kuongeza uzalishaji katika sekta asili (primary production) ili kukidhi mahitaji na usalama wa chakula na upatikanaji wa mazao ghafi kwa uzalishaji viwandani kwa bei itakayowezesha ushindani kimataifa