National Economic Survey
Permanent URI for this communityhttp://10.1.67.219/handle/123456789/10
Browse
Browsing National Economic Survey by Subject "Maendeleo ya Taifa"
Now showing 1 - 2 of 2
- Results Per Page
- Sort Options
Item Hali ya Uchumi 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016-17(Wizara ya Fedha na Mipango, 2016) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee na kujadili Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17. Pamoja na hotuba hii nawasilisha vitabu vya Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17. Taarifa ya Hali ya Uchumi na Mpango ninayowasilisha ndio msingi wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17Item Hali ya Uchumi wa Taifa 2023(Wizara ya Fedha, 2024-06) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMwaka 2023, Pato halisi la Taifa lilifikia shilingi bilioni 148,399.76 kutoka shilingi bilioni 141,247.19 mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asimilia 4.7 mwaka 2022. Ukuaji huo ulichangiwa na: jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi pamoja na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu na usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi. Hata hivyo, kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa cha asilimia 5.1 mwaka 2023 kipo chini ya lengo la mwaka la asilimia 5.2. Hii ilitokana na: kupanda kwa gharama za uzalishaji katika baadhi ya sekta; mabadiliko ya tabianchi yaliyoathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini na kuharibu miundombinu ikiwemo madaraja na barabara; pamoja na hatua zilizochukuliwa na nchi zilizoendelea katika kukabiliana na mfumuko wa bei zilizosababisha kuongezeka kwa gharama za mikopo kutoka masoko ya kimataifa ya fedha na hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji.