National Economic Survey
Permanent URI for this communityhttp://10.1.67.219/handle/123456789/10
Browse
Browsing National Economic Survey by Subject "Hali ya uchumi wa Taifa"
Now showing 1 - 5 of 5
- Results Per Page
- Sort Options
Item Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015(Wizara ya Fedha na Mipango, 2015) Tanzania, United RepublicItem Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018(Wizara ya Fedha na Mipango, 2019) Tanzania, United RepublicMwaka 2018, Serikali kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilifanya maboreshoya takwimu za Pato la Taifa kwa kutumia mwaka 2015 kama mwaka wa kizio kutoka mwaka wa kizio wa 2007. Kufuatia maboresho hayo, mabadiliko kadhaa yalijitokeza ikiwemo mfumo na ukubwa wa Pato la Taifa; viwango vya ukuaji na mchango wa sekta mbalimbali katika Pato la Taifa; na uwiano wa viashiria mbalimbali kwa Pato la Taifa. Maelezo ya kina kuhusu maboresho hayo yako katika sura ya kumi. Kutokana na zoezi hilo, kuanzia toleo hili takwimu zitakazotumika zitakuwa za mwaka wa kizio wa 2015. Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017. Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo. Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na: sanaa na burudani iliyokua kwa asilimia 13.7; ujenzi (asilimia 12.9); uchukuzi na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na habari na mawasiliano (asilimia 9.1).Item Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2019(2019) Tanzania, United RepublicPato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 mwaka 2019 kama ilivyokuwa mwaka 2018. Ukuaji huu ulitokana na kuendelea kuimarika kwa sekta ya madini, kuboreshwa kwa huduma za usafiri na usafirishaji, pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege, miradi ya nishati ya umeme pamoja na ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya. Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji mwaka 2019 ni pamoja na: madini iliyokua kwa asilimia 17.7; ujenzi (asilimia 14.8); sanaa na burudani (asilimia 11.2); na usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 8.7).Item Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020(Wizara ya Fedha na Mipango, 2021) Tanzania, United RepublicMwaka 2020, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2019. Kupungua kwa kasi ya ukuaji kulitokana na: mvua zilizozidi wastani ambazo zilisababisha uharibifu wa miundombinu ya usafirishaji nchini na kuchelewesha utekelezaji wa baadhi ya miradi; na athari za hatua zilizochukuliwa na mataifa mbalimbali duniani ambao ni washirika wakubwa wa biashara wa Tanzania katika kukabiliana na janga la UVIKO-19. Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na mataifa hayo ni pamoja na kufunga mipaka, kusitisha safari za ndege za kimataifa na kusitisha baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazohusisha mikusanyiko. Hatua hizo zilisababisha uchumi wa dunia kuporomoka mwaka 2020 ambapo nchi nyingi zilikuwa na ukuaji hasi na kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni nchi 11 tu zilikuwa na ukuaji chanya kati ya nchi 45. Pamoja na kupungua kwa kasi ya ukuaji, Tanzania iliweza kuwa na ukuaji chanya kutokana na kutochukua hatua za kuzuia kufanyika kwa shughuli za kiuchumi isipokuwa kwa kipindi kifupi tu cha robo ya pili ya mwaka 2020 ambapo ilisitisha kwa muda baadhi ya shughuli zinazohusisha mikusanyiko ya watu kama shule, sanaa na burudani. Athari za janga la UVIKO-19 zilijitokeza zaidi katika shughuli za kiuchumi za malazi na huduma ya chakula pamoja na sanaa na burudani ambazo zilikuwa na ukuaji hasi mwaka 2020.Item Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Tanzania, United RepublicMwaka 2021, thamani halisi ya Pato la Taifa ilifikia shilingi milioni 135,517,812.70 ikilinganishwa na shilingi milioni 129,130,182.02 mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 4.9 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 mwaka 2020. Kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji kulitokana na: uwekezaji wa kimkakati hususani katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, ujenzi wa barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini hususani dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo katika sekta binafsi ambayo imechochea shughuli za kiuchumi. Sekta zilizokua kwa viwango vikubwa katika kipindi husika ni pamoja na: sanaa na burudani (asilimia 19.4); umeme (asilimia 10.0); madini (asilimia 9.6); na habari za mawasiliano (asilimia 9.1). Sekta za malazi na huduma ya chakula pamoja na sanaa na burudani ambazo mwaka 2020 ziliathiriwa kwa kiasi kikubwa na UVIKO - 19 zilianza kukua kwa viwango chanya mwaka 2021 kufuatia kuimarika kwa huduma za utalii ambazo zina mchango mkubwa katika sekta hizo.