National Economic Survey
Permanent URI for this communityhttp://10.1.67.219/handle/123456789/10
Browse
Browsing National Economic Survey by Subject "Hali ya Uchumi"
Now showing 1 - 7 of 7
- Results Per Page
- Sort Options
Item Hali ya Uchumi 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2016-17(Wizara ya Fedha na Mipango, 2016) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee na kujadili Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17. Pamoja na hotuba hii nawasilisha vitabu vya Taarifa ya Hali ya Uchumi kwa Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17. Taarifa ya Hali ya Uchumi na Mpango ninayowasilisha ndio msingi wa bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17Item Hali ya Uchumi wa Taifa 2023(Wizara ya Fedha, 2024-06) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMwaka 2023, Pato halisi la Taifa lilifikia shilingi bilioni 148,399.76 kutoka shilingi bilioni 141,247.19 mwaka 2022, sawa na ukuaji wa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asimilia 4.7 mwaka 2022. Ukuaji huo ulichangiwa na: jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi pamoja na uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu na usafirishaji; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya mawe; na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi iliyochachua shughuli za kiuchumi. Hata hivyo, kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa cha asilimia 5.1 mwaka 2023 kipo chini ya lengo la mwaka la asilimia 5.2. Hii ilitokana na: kupanda kwa gharama za uzalishaji katika baadhi ya sekta; mabadiliko ya tabianchi yaliyoathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini na kuharibu miundombinu ikiwemo madaraja na barabara; pamoja na hatua zilizochukuliwa na nchi zilizoendelea katika kukabiliana na mfumuko wa bei zilizosababisha kuongezeka kwa gharama za mikopo kutoka masoko ya kimataifa ya fedha na hivyo kuathiri shughuli za uzalishaji.Item Hali ya Uchumi wa Taifa Katika Mwaka 2022(Wizara ya Fedha na Mipango, 2022) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMwaka 2022, thamani halisi ya Pato la Taifa ilifikia shilingi milioni 141,872,730 ikilinganishwa na shilingi milioni 135,478,189 mwaka 2021, sawa na ukuaji wa asilimia 4.7. Kiwango hicho cha ukuaji kilitokana na: mikakati iliyochukuliwa na Serikali kukabiliana na athari za vita nchini Ukraine; uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati, maji, afya, elimu, barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwamuzalishaji wa madini, hususan makaa ya mawe, jasi, chumvi, almasi, mawe ya chokaa na shaba; na kuongezeka kwa shughuli za utalii. Hata hivyo, kiwango cha ukuaji kilipungua kwa nukta ya asilimia 0.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.9 mwaka 2021 kutokana na athari ya vita kati ya Urusi na Ukraine iliyosababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji katika baadhi ya sekta pamoja na mabadiliko ya tabianchi yaliyoathiri uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa baadhi ya maeneo nchini. Aidha, sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji mwaka 2022 ni pamoja na: sanaa na burudani iliyokua kwa asilimia 19.0; madini (asilimia 10.9); fedha na bima (asilimia 9.2); malazi na huduma ya chakula (asilimia 9.0) na umemeItem Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016(Wizara ya Fedha na Mipango, 2016) Tanzania, United RepublicMwaka 2016, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.0, sawa na ilivyokuwa mwaka 2015. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na: kuongezeka kwa ufuaji wa umeme hususan utokanao na gesi asilia; kuongezeka kwa uzalishaji viwandani; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi kufuatia kuanza kwa sera ya Serikali ya kutoa elimu msingi bure iliyoanza Januari 2016. Katika kipindi hicho, shughuli za uchumi zilizokua kwa viwango vikubwa ni pamoja na: ujenzi asilimia 13.0; habari na mawasiliano (asilimia 13.0); usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na uchimbaji madini na mawe (asilimia 11.5). Aidha, shughuli za kiuchumi za kilimo zilikua kwa kasi ndogo ya asilimia 2.1 mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 2.3 mwaka 2015 kutokana na kutokuwa na mvua za kutosheleza katika msimu wa kilimo wa 2015/16.Item Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017(Wizara ya Fedha na Mipango, 2017) Tanzania, United RepublicMwaka 2017, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.1ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2016. Ukuaji huu ulitokana na utekelezaji wa miradi ya miundombinu ikiwemo miundombinu ya maji, nishati, barabara, reli na viwanja vya ndege sambamba na kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya madini kama almasi na makaa ya mawe na kuimarika kwa sekta ya kilimo. Katika kipindi hicho, shughuli za uchumi zilizokua kwa viwango vikubwa ni pamoja na: uchimbaji madini na mawe (asilimia 17.5); maji (asilimia 16.7); usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 16.6); habari na mawasiliano (asilimia 14.7); na ujenzi asilimia 14.1. Aidha, kasi ya ukuaji katika sekta ya kilimo ambayo inaajiri asilimia 66.3 ya kaya nchini na kuchangia asilimia 20 ya mauzo nje iliongezeka mwaka 2017 kufikia asilimia 3.6 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 2.1 mwaka 2016. Hata hivyo, kulikuwa na kasi ndogo ya ukuaji kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi kama vile huduma za fedha na bima, na utawala na ulinzi na utawala (asilimia 6.4)Item Speech By the Minister for Finance and Planning, Hon. Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (MP.), Presenting to The Parliament, The Economic Survey 2022 Report and The National Annual Development Plan 2023- 2024(Ministry of Finance and Planning, 2023) Tanzania, United RepublicItem Taarifa ya Hali ya Uchumi 2008 na Malengo katika Kipindi cha Muda wa Kati 2009 - 2012(Wizara ya Fedha na Uchumi, 2008) Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa likae kama Kamati ili liweze kupokea na kujadili Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2008 na malengo katika kipindi cha Muda wa Kati (2009/10 – 2011/12). Pamoja na hotuba hii, nawasilisha Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2008; na Kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2009/10.